Orkonerei FM

Wazazi wahimizwa kutoa michango ya shule kwa wakati.

20 March 2024, 4:51 pm

Shule ya Msingi Terrrat Simanjiro, Picha na Joyce Elius.

Kikao cha wazazi na uongozi wa shule wa msingi Terrat Wilaya ya Simanjiro kimeazimia kushirikiana kuhakikisha kutatua changamoto zilizopo shuleni hapo ikiwepo tatizo la upungufu wa walimu.

Na Joyce Elius, Terrat.

Kikao hicho kilichofanyika tarehe 19.03.2024 kimeongozwa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Mwl Deo Lusian ambaye amebainisha kuwa lengo la kikao hicho cha Wazazi ni kujadili changamoto na maendeleo ya shule hiyo.

Mwalimu Deo amesema kuwa maendeleo ya shule kitaaluma sio mabaya na wanapambana kwa kadiri wanavyoweza kwa kushirikiana na viongozi na wazazi ili kufikia malengo.

Sauti ya Mwl Deo Lusian,Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Terrat, Simanjiro.

Aidha mwalimu Deo amebainisha kuwa shule imekuwa na utaratibu wa  chakula cha mchana shuleni kwa ajili ya wanafunzi kwa kuchangiwa na wazazi japo kumekuwepo na changamoto ya baadhi ya wazazi kutokuchangia kwa wakati au kushindwa kabisa kuchangia.

Sauti ya Mwl Deo Lusian,Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Terrat, Simanjiro.

Mtendaji wa Kijiji cha Terrat Bw Minas Hamisi Juma amesema kuwa uongozi wa kijiji hautasita kumchukulia hatua za kisheria mzazi au mlezi yeyote atakayekaidi azimio la kupeleka chakula shuleni kwa ajili ya mwanafunzi.

Sauti ya Minas Hamisi Juma, afisa mtendaji kijiji cha Terrat.

Naye diwani wa Kata ya Terrat Mh Jackson Materi amesema kuwa shule ya msingi ya Terrat inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwepo la upungufu wa walimu na nyumba za walimu,

Mheshimiwa Jackson Materi,Diwani kata ya Terrat.

Baadhi ya Wazazi walioshiriki kikao hicho Israel Mesiaki na Shakila Hamadi amesema kuwa kikao kimekwenda vizuri na kuwasihi wazazi kuchangia michango yote husika kwa ajili ya wanafunzi na maendeleo ya shule.

Sauti ya Wazazi, Israel Mesiaki na Shekila Hamadi.

Shule ya Msingi ya Terrat ni miongoni mwa shule kongwe ndani ya Wilaya ya Simanjiro ina wanafunzi 977, walimu 7, na vyumba vya madarasa 9 tu, hivyo ina upungufu wa walimu 13 na vyumba vya madarasa 11.

Sehemu ya Wazazi waliohudhuria kikao cha Wazazi na uongozi wa shule ya msingi Terrat.