Orkonerei FM

Je, kuna nafasi sawa ya kijinsia katika kumiliki ardhi?

8 May 2024, 3:04 pm

Na Dorcas Charles

 Baadhi ya maeneo na jamii zimekua haziamini mwanamke katika kumilikisha ardhi na hii inatokana na mila na desturi za jamii husika.

Lakini sera ya taifa   ya ardhi ya mwaka 1995 inatambua kuwa wanawake na wanaume wana haki sawa yakupata, kumiliki, kutumia na kuuza ardhi, sera hii inalenga kuboresha hali ya wanawake katika maswala ya ardhi.

Baadhi ya wananchi wametoa maoni yao wakieleza kama kuna haki sawa ya kijinsia katika kumilikia ardhi kwenye maeneo yao.

Kwa upande wake Msaidizi wa kisheria kutoka shirika lisilo la kiserikali SELA Bw. HASSAN FUSSA amesema ni haki ya kila mtu kumiliki ardhi bila kuzingatia jinsi yake.