Orkonerei FM

Akina mama wa kijiji cha Emboreet wilaya ya Simanjiro wapata ahueni Upatikanaji wa maji safi.

22 March 2023, 9:20 am

Mtoto akichota maji bombani (picha kwa msaada wa Mtandao)

Siku ya maji duniani huadhimishwa kila mwaka na mwaka hu imeadhimishwa Machi 22, 2023 na huwa ni mahususi kwa kuangalia upatikanaji wa maji safi na salama laki pia usalama wa maji.

Na Isack Dickson

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Dkt.Suleiman Serera amezindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Emboreet kata ya Emboreet wilaya ya Simanjiro ikiwa ni wiki ya maji kidunia.

Kama ujuavyo akinamama ndiyo huwa na jukumu kubwa la kuhakikisha maji yapo nyumbani wakati wote haswa katika jamii ya kimaasai ambayo ndiyo kubwa katika kijiji hiki cha emboreet fuatana na Isack Dickson katika makala fupi hii ili kufahamu uzinduzi huo ulikuwa vipi?