Orkonerei FM

Unakabiliana vipi na tamaduni zinazomnyima mwanamke fursa ya kushiriki katika mijadala?

8 March 2024, 6:27 pm

Wananchi wa kijiji cha Terrat wakikamilisha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani

leo ni siku ya maadhisho ya wanawake duniani na kauli mbiu ya mwaka huu inasema ” Wekeza kwa mwanamke kuharakisha maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii”

Bado kuna mifumo dume na mila potofu  zinazoweka vikwazo na masharti kwa wanawake kuhusu namna wanavyopaswa kuongea kuvaa na kujihusisha na jamii.

Wanawake wamekua na majukumu mengi ya kifamilia na kazi za nyumbani zinazowabana na kuwanyima muda wa kushiriki  katika mijadala.

Karibu kusikiliza mjadala ambao umefanywa na Dorcas Charles kuhusu “kushirikiana kwenye kazi/ majukumu ya nyumbani kutamuwezesha vipi mwanamke kupata fursa ama muda wa kushiriki kwenye mijadala?”