Orkonerei FM

Mafunzo ya matumizi ya mtandao kwa watangazaji wa Orkonerei FM Redio

13 December 2023, 5:25 am

Mkufunzi wa mafunzo kutoka TADIO Bw Amua Rushita na watangazaji wa Orkonerei FM wakiwa darasani, Picha na Baraka Ole Maika.

Mafunzo ya Matumizi ya Mtandao kwa redio wanachama wa mtandao wa vyombo vya habari vyenye maudhui ya kijamii nchini Tanzania TADIO yameendelea kushika kasi katika vituo vya redio zilizopo kanda ya kaskazini.

Na Baraka David Ole Maika,

Mafunzo ya matumizi ya Mtandao maarufu kama portal kwa redio wanachama wa TADIO yameendelea katika vituo vya redio wanachama wa mtandao huo kanda ya kaskazini.

Akiendesha mafunzo hayo katika kituo cha redio cha Orkonerei FM mmoja wa wakufunzi kutoka TADIO Bw Amua Rushita amesema kuwa lengo la TADIO ni kuwezesha redio wanachama wa mtandao wa TADIO kutanua wigo wao wa usikivu na kutumia fursa hiyo kupata matangazo na kujingizia kipato.

Mmoja wa watangazaji wa Orkonerei FM Radio Isack Dickson amesema kuwa mafunzo hayo kutoka TADIO ni muhimu sana kwa redio za kijamii zilizopo pembezoni kwani hazifahamiki kwa kiasi kikubwa na haziwafikii wadau wengi ila kupitia mtandaoni zitatanua wigo wa kufahamika na kuwafikia wadau wengi zaidi.

Sauti ya Issack Dickson, mtangazaji wa Orkonerei FM Radio

Naye msimamizi wa vipindi wa Orkonerei FM Radio Bi Dorcus Charles amesema kuwa mafunzo hayo ya matumizi ya mtandao wa portal yana manufaa kwa waandishi wa habari, watangazaji na vituo vya redio kwa sababu redio itatanua wigo wa usikivu na watangazaji nao watapata fursa ya kufahamika kupitia maudhui na vipindi watakazochapicha na kuweka mtandaoni.

Sauti ya Dorcus Charles, msimamizi wa vipindi Orkonerei FM Radio.

Mafunzo hayo ya matumizi ya mtandao kwa redio wanachama wa TADIO ambayo yamefanyika nje na ndani ya vituo yamejumuisha redio wanachama wa mtandao huo kutoka mkoa wa Manyara, Arusha na Kilimanjaro, ikiwepo Orkonerei FM Radio, Triple A FM, Radio Loliondo, FM Manyara na Boma Hai FM.