Orkonerei FM

Jamii wahimizwa kujitokeza kuchanjwa chanjo ya UVIKO-19

8 December 2023, 4:40 pm

Chanjo ya COVID 19. Picha kwa hisani ya Mwananchi.

Jamii wametakiwa kujitokeza kuchanjwa chanjo ya UVIKO19 ili kukabiliana na Maambukizi ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona.

Na Baraka David Ole Maika

Wito huo umetolewa na Mratibu wa Chanjo Wilaya ya Simanjiro Bw Hassan Bakari Keya alipofanya mahojiano na Orkonerei FM Redio.

Bwana Hassan Bakari Keya akibainisha kuwa Chanjo ya ugonjwa wa virusi vya Korona ni Mfumo wa kibaolojia uliotengenezwa mahususi kuwezesha Mwili kupambana dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO19.

Sauti ya mratibu wa chanjo wilaya ya Simanjiro Bw Hassan Keya alipohojiwa na Baraka Ole Maika.

Aidha Bw Hassan Keya amebainisha mkakati wa wilaya katika kukabiliana na taarifa na maneno potofu kuhusu ya chanjo ya UVICO-19.

sauti ya mratibu wa chanjo wilaya ya Simanjiro Bw Hassan Keya alipohojiwa na Baraka Ole Maika.

Pamoja na jitihada kubwa inayofanya na Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro kuhamasisha jamii kupata chanjo ya UVIKO-19 bado jamii ya Wafugaji wengi wa wilaya hiyo kwa asilimia kubwa hawajapata chanjo ya UVIKO-19 kutokana na mfumo wa maisha yao ya kuhamahama na mifugo kufuata malisho kutoka eneo moja kwenda jingine.