Orkonerei FM

Nini chanzo cha idadi ndogo ya wanafunzi kidato cha kwanza kata ya Terrat?

20 January 2024, 1:46 pm

Waliohudhuria shuleni ni wengi lakini si wote kwani waliofaulu wote wanatakiwa kuripoti shule.

Na Mwandishi wetu.

Ni wiki ya pili sasa tangu wanafunzi wa kidato cha kwanza kutakiwa kuripoti shuleni nchi nzima  kwa shule ya sekondari Terrati wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ambayo imepangiwa kuwapokea wanafunzi 226, wavulana wakiwa 101 na wasichana 125 lakini waliokwisha kuripoti ni wanafunzi 171 ikiwa ni jumla ya wasichana 90 na wavulana 81 sawa na asilimia 75.6.

Ili kufahamu hali ilivyo kuhusu wanafunzi wa kidato cha kwanza waliokwisha kuripoti shuleni haswa Shule ya Upili ya Terrat ,karibu kusikiliza makala (kipindi) hii..