Orkonerei FM

Mfumko bei ya mahindi waitesa Simanjiro

7 December 2023, 2:11 pm

Wachuuzi na Wanunuzi wa mahindi sokoni, Picha na Gazeti la Mwananchi.

Mfumko wa bei kwa mazao ya nafaka hasa mahindi umeendelea kuwa changamoto kwa jamii ya wafugaji wilayani Simanjiro mkoani Manyara kutoka shilingi 7,000 hadi shilingi 15,000 hali inayosababisha baadhi ya familia kushindwa kumudu gharama za kununua mahindi kwa matumizi ya nyumbani.

Na Isack Dickson

Baadhi wa wananchi wa kijiji cha Terrat kilichopo kata ya Terrat wilayani Simanjiro waliozungumza na Orkonerei FM Redio, wamebainisha kuwa bei ya mahindi ipo juu sana tofauti na mwaka uliopita wa 2022 hali inayopelekea baadhi ya familia kushindwa kumudu gharama ya kununua mahindi hivyo kukosa chakula nyumbani.

Mwandishi wetu Isack Dickson ametembelea soko la Terrat na kutuandalia taarifa hii.

Sauti za wananchi wa kijiji cha Terrat, Simanjiro walipohojiwa na Isack Dickson.