Orkonerei FM

Dkt.Serera Mgeni rasmi kilele wiki ya maji Simanjiro.

19 March 2024, 8:59 pm

“Kwanini tumechagua Terrat kufanyika kilele cha wiki ya maji kwanza tumetekeleza mradi wa maji hivi karibuni ,lakini kingine ni utayari wa kwanzia ofisi za wilaya hadi huku chini lakini pia na ratiba yetu”Mhandisi Joanes Martin Meneja RUWASA Simanjiro.

Na Mwandishi wetu.

Meneja RUWASA wilaya ya Simanjiro Mhandisi Joanes Martin amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu ya wiki ya maji ambayo huwa yanafanyika kila mwaka kilele chake kikiwa Tar.22 mwezi Machi kiwilaya yatafanyika katika kata ya Terrat kwa Wilaya ya Simanjiro.

Akizungumza katika kipindi cha Tingatinga kinachoruka kupitia radio Orkonerei fm amesema kuwa kutakuwa na shughuli mbalimbali katika kuelekea kilele cha wiki ya maji ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya ulipaji wa ankara za maji,kusikiliza kero za watumia maji pamoja na kuzindua miradi ya maji iliyokwisha kutekelezwa.

Aidha amesema kuwa utekelezaji wa miradi ya maji hadi sasa kwa mwaka wa fedha 2023/24 ni zaidi ya asilimia 70 na zilitengwa fedha kiasi cha shilingi bil.2.4 ili kufanikisha miradi 8 ya maji katika wilaya ya simanjiro.

karibu kusikiliza sehemu ya Mahojiano hayo (makala).