Orkonerei FM

Wanawake wanashiriki vipi katika kufanya maamuzi ya familia?

8 February 2024, 7:12 pm

Wanakijiji wa kijiji cha Terrati Simanjiro mkoani Manyara

Mwandishi wetu akifanya mahojiano na mwenyekiti wa Malaigwani wilaya ya Simanjiro Lesira Samburi.

Mwanamke amekuwa akikosa nafasi ya kutoa maamuzi ngazi ya familia ikisemekana sababu kubwa ni mila na desturi za jamii mbalimbali nchini Tanzania.

Jamii hizo zimeaswa kuwa na ushirikiano wa kufanya maamuzi ndani ya familia ili kujenga familia iliyo bora.

Karibu kusikiliza kipindi cha nijuze ambapo utapata elimu na mada kuu katika kipindi hiki ni wanawake wanashiriki vipi katika kufanya maamuzi ya familia?