Orkonerei FM

Kufanya mazoezi pamoja kwatajwa kuongeza ushirikiano

14 December 2023, 11:41 am

[picha kwa msaada wa mtandao]

Kwanza michezo inaleta watu pamoja, kufahamiana kuleta ule undugu …pia mazoezi yanaongeza muda wa kuishi” Mratibu ndg. Mbaga

Na Isack Dickson

Mratibu wa michezo wilaya ya simanjiro mkoa wa manyara bwana CHARLES MSENGI MBAGA Amesema kuwa wilaya ya simanjiro inaandaa program jumuishi ya kufanya mazoezi ili kuendelea kuimarisha afya.

Akizungumza na Radio Orkonerei fm kwanjia ya simu ndg. MBAGA amesema kuwa wapo katika harakati za kuandaa mpango huo na mara baada ya kuukamilisha watauwasilisha ofisi ya mkuu wa wilaya ya simanjiro ili uweze kutekelezwa.

Kadhalika ndg. MBAGA amesema kuwa kushiriki michezo kama jamii kutajenga ushirikiano mkubwa pamoja na kujenga afya ili kupunguza matokeo ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.