Orkonerei FM

Unatumiaje ukame kujipatia kipato?

4 July 2024, 11:02 am

Mkulima wa Bustani ya Mbogamboga akimwagilia mboga aina ya Kabichi. (Picha na Isack Dickson).

Nijuze Radio Show.

Jamii nyingi za kifugaji zinaishi katika maeneo yaliyombali na miundombinu ya umeme, masoko hivyo zinakabiliwa na changamoto za kupata rasilimali na fursa za kuboresha kipato chao kipindi cha ukame,hali inayopelekea kutegemea shughuli moja tu ya kifugaji kujiingizia kipato ambapo wakati wa ukame ufugaji ukumbwa na changamoto nyingi kutokana na kutokuepo kwa malisho na maji kwaajili ya mifugo.

Katika makala hii ya nijuze ambayo hukujia kila Alhamisi saa 12:00 Jioni ikiwa na marudio yake siku ya Jumamosi saa 4:30 Asubuhi inaangazia namna mkulima ama mfugaji na mwanajamii unaweza kujiingizia kipato wakati wa ukame.Karibu kuisikiliza.