Orkonerei FM

Mafunzo ya Usimamizi na Utunzaji wa Misitu.

8 November 2021, 1:35 pm

08.11.2021

Na Baraka David Ole Maika:

Viongozi wa Vijiji na Wasimamizi wa Misitu 55 kutoka Wilaya Ngorongoro wamepatiwa Mafunzo ya Usimamizi na Utunzaji wa Misitu.

Mafunzo hayo ya Siku Tatu yamefanyika katika Chuo cha Misitu olmotonyi iliyopo Ngaramtoni Halmashauri ya Wilaya ya Arusha chini ya Ufadhili wa Shirika la Frankfout Zoological Society.

Akizungumza na Orkonerei FM Radio Meneja wa Mradi kutoka Shirika la Frankfout Zoological Society Bw Masegeri Tumbuya amesema kuwa Lengo la Mafunzo hayo ni kuwawezesha Washiriki kupata elimu ya jinsi ya kulinda na kutunza misitu ambayo ni muhimu kwa maisha ya jamii, mifugo na ikolojia ya Hifadhi ya Serengeti.

Usimamizi na utunzaji wa Misitu.