Orkonerei FM

Umuhimu wa matumizi ya choo bora

28 June 2024, 11:16 am

Kwa mujibu wa Ripoti ya Tafiti ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria ya Mwaka 2022 yaani (Demographic and Health Survey and Malaria Indicator Survey) imeonesha kuna ongezeko kubwa la watu wanaotumia vyoo bora kutoka asilimia 21 mwaka 2016 hadi asilimia 74.8 mwaka 2022.

Takwimu hizi ni hatua chanya katika kufikia lengo la 6.2 la SDG ifikapo mwaka 2030, mkoa unaoongoza kwa matumizi ya vyoo bora ni Dar es Salaam (98.5%),Hata hivyo, bado kuna changamoto, kwani asilimia 9.8 ya watu nchini hawana vyoo kabisa, hasa katika maeneo ya vijijini.

Mkoani Manyara, utafiti huo unaonesha kuwa, asilimia ya watu wanaotumia vyoo bora ni 22.3 pekee. Katika makala hii ya Kurunzi tunaona ni kwanini vyoo havitumiki kwa kiwango kikubwa katika mkoa wa Manyara haswa wilaya ya Simanjiro. KARIBU KUISIKILIZA!!!