Orkonerei FM

NCAA yapokea gari la kutatua migogoro kati ya binadamu, wanayamapori

9 March 2024, 10:09 am

Wafanyakazi wa mamlaka ya uhifadhi Ngorongoro NCAA pamoja na wale wa Gardworld Tanzania wakiwa pembeni ya gari walilokabidhiana. (picha na mamlaka ya NCAA).

Na mwandishi wetu.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongro (NCAA) imepokea gari aina ya Suzuki Jimny kutoka shirika lisilo la kiserikali la Elephant Protection Initiative (EPI) ya nchini Uingereza kupitia mbia wake Kampuni ya ulinzi ya GardaWorld Tanzania kwa lengo la kusaidia kupunguza Migogoro kati ya wanyamapori na wananchi.

Akipokea gari hiyo kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi NCAA, kaimu meneja wa huduma za Ulinzi NCAA SCO Donatus Gadiye ameeleza kuwa gari hiyo imetolewa kwa ajili kuimarisha ulinzi na kupunguza migogoro kati ya wanyamapori na wananchi wanaozunguka hifadhi ya Ngorongoro hasa kwa wanyama wakali kama tembo kuvamia mashamba ya wananchi.

Mkurugenzi wa GardWorld tawi la Tanzania Tommy Bright  ameeleza kuwa taasisi yao imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali inayolenga ulinzi wa Wanyamapori kwa ajili ya kupunguza migogoro kati ya Wanyamapori na binadamu na kuangalia njia mbalimbali za kisasa katika kupambana na hali hiyo.