Orkonerei FM

“Nilikatwa Mkono, Lakini Sikukata Tamaa – Simulizi ya Veronica Kidemi”

17 June 2026, 3:17 pm

Na Mwandishi Wetu Nyangusi Ole Sang’ida

Wakati mwingine maisha hubadilika kwa sekunde chache tu sekunde zinazoweza kuacha majeraha yasiyofutika na kumbukumbu za maisha yote.Leo tunakuletea simulizi ya mwanamke jasiri aliyepitia tukio la kusikitisha mwaka 2020, lakini akaamua kusimama tena na kuendelea na maisha.

Kabla hatujaingia ndani ya simulizi yake, hebu kwanza tusikie kutoka kwake mwenyewe yeye ni nani, na anajitambulishaje kwa jamii?

Baada ya kujitambulisha, Veronica anaanza kwa kueleza kuhusu ukatili wa kijinsia anasema wengi huufahamu kwa upande mmoja tu, ilhali una sura nyingi zikiwemo ukatili wa kimwili, kisaikolojia, kiuchumi na kingono.Veronica anakiri kuwa katika maisha yake amewahi kukumbana na aina mbalimbali za ukatili huo.

Baada ya kueleza maana ya ukatili wa kijinsia, Veronica anafungua ukurasa mgumu zaidi wa maisha yake, ukurasa wa tukio lililobadilisha maisha yake mwaka 2020. Anasema hadi leo bado hupata ugumu kueleza kila kilichotokea kutokana na namna tukio hilo lilivyokuwa la ghafla na la kutisha.

Hebu tusikilize simulizi yake.

Licha ya maumivu aliyoyapitia Veronica hakuruhusu ndoto zake kufa akiwa mwalimu, alikabiliwa na changamoto ya kuendelea kufundisha baada ya kupoteza mkono wake wa kulia. Hata hivyo, aliamua kuanza upya kwa kujifunza kuandika kwa mkono wa kushoto.

Kwa upande wake Mweka Hazina wa Voice of Women Africa, Happy Satian Mollel anasisitiza kuwa familia bora na kizazi bora hujengwa kwa misingi ya upendo, heshima na usalama si ukatili.

Tunapoufikia mwisho wa simulizi yake Veronica anatoa ujumbe kwa jamii anaamini migogoro inaweza kutatuliwa kwa mazungumzo badala ya ukatili, kwani ukatili huacha maumivu, chuki na athari zinazoweza kuendelea hata kwa kizazi kijacho.

Hiyo ndiyo simulizi ya Veronica Kidemi, mwanamke ambaye licha ya kupitia maumivu makubwa, hakukubali kukata tamaa. Simulizi yake ni ushuhuda wa ujasiri, matumaini na nguvu ya kuanza upya.

Baada ya kusikia simulizi hii wewe una maoni gani? Unadhani jamii inapaswa kufanya nini ili kutokomeza ukatili wa kijinsia?