Orkonerei FM
Orkonerei FM
26 May 2026, 2:39 pm
Na Joyce Elius

Picha ya kadi ya Kliniki ya mtoto.
Wazazi na walezi Wilayani Simanjiro wameshauriwa kuzingatia matumizi sahihi ya kadi za kliniki za watoto ili kurahisisha ufuatiliaji wa afya na makuzi yao, hatua itakayosaidia kuepusha vifo na magonjwa yanayoweza kuzuilika.
Wito huo umetolewa na Afisa Ustawi wa Jamii wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani, Bi. Nambaya Nakapala, wakati akizungumza kuhusu umuhimu wa kadi hizo katika ustawi wa mtoto.
Akizungumza na Joyce Elius kuptia kipindi cha Mchaka Mchaka kinachoruka Orkonerei Fm Radio Bi. Nambaya amesema Kadi ya kliniki inamsaidia mzazi kufuatilia chanjo alizopata mtoto, tarehe za chanjo zinazofuata, na kuzuia kurukwa kwa chanjo hizo.