Orkonerei FM

Ongezeko la Vituo vya Afya Lachochea Akina Mama Kujifungulia Hospitalini

19 June 2026, 9:13 am

Ongezeko la vituo vya afya katika maeneo mbalimbali limeongeza upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi kwa kuwafikishia wananchi huduma karibu zaidi. Hali hii imechangia akina mama wengi kuchagua kujifungulia hospitalini kwa urahisi na usalama zaidi.

Kurunzi Maalum

Uwekezaji unaoendelea katika sekta ya afya, hususan ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya katika maeneo mbalimbali, umeendelea kuleta matokeo chanya katika huduma za afya ya uzazi. Kuongezeka kwa vituo vya afya karibu na wananchi kumesaidia kupunguza umbali ambao wajawazito walilazimika kusafiri ili kupata huduma za kujifungua salama.

Katika kipindi hiki maalum, wanawake waliojifungulia katika vituo vya afya na hospitali wametoa ushuhuda kuhusu faida walizopata kwa kupata huduma chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya. Wamesema uwepo wa vituo vya afya vilivyo karibu na makazi yao umeongeza urahisi wa kufika hospitalini wakati wa kujifungua na hivyo kupunguza hatari zinazoweza kujitokeza wakati wa uzazi.