Orkonerei FM

Umuhimu wa klinik ya mtoto wakati wote

12 December 2025, 8:16 pm

picha kwa msaada wa AI

Na mwandishi wetu Evanda Barnaba

Kuhudhuria maadhurio ya kliniki ya mtoto ni jambo la muhimu sana kwa mzazi, kwani ni fursa ya kipekee ya kufuatilia maendeleo ya afya ya mtoto wako. Kliniki inatoa nafasi ya kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa afya kuhusu lishe, chanjo, na matatizo ya kiafya yanayoweza kujitokeza. Aidha, ni wakati mzuri wa kujibu maswali yako na kupata ufahamu zaidi kuhusu jinsi ya kumlea mtoto kwa afya njema.

Kwenye kipindi cha Kurunzi Maalum kinachorushwa kila Ijumaa saa mbili na nusu asubuhi hapa Orkonerei FM, mwandishi Evanda Barnaba amezungumza na wataalamu mbalimbali na wananchi kuhusu umuhimu wa kuhudhuria klinik ya mtoto wakati wote.