Orkonerei FM

Halmashauri ya Arusha yakopesha zaidi ya Tsh mil. 596 bila riba

22 May 2026, 12:10 pm

Na Nyangusi Olesang’ida

Halmashauri ya Wilaya ya Arusha imetoa jumla ya Shilingi milioni 596,000,000 kama mikopo isiyo na riba kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026, inayolenga kuyawezesha makundi maalum kiuchumi ikihusisha vikundi 18 vya wanawake, vikundi 26 vya vijana, na vikundi 10 vya watu wenye ulemavu.

Akizungumza Na Orkonerei Fm Radio Mapema leo kwenye kipindi cha Kurunzi Mtaani, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri hiyo, Stedvant Kileo, amebainisha kuwa mikopo hiyo itasaidia kuongeza uzalishaji na kuimarisha viwanda vidogo vinavyomilikiwa na wanavikundi hao, huku kukiwa na utaratibu rafiki wa marejesho kuanzia kipindi cha mpito cha miezi mitatu hadi miaka miwili.

Picha ya wanakikundi wakisubiri kuanza kwa utoaji wa mikopo minne Mkoani Arusha, Piicha na Nyangusi Olesang’ida

Kupitia ushuhuda wa vikundi vya Arusha Dairy na Fahari ya Mwanamke, imebainika kuwa Halmashauri ya Jiji la Arusha inatoa mikopo ya mamilioni ya fedha kwa mchakato ulio wazi kabisa ili kukuza ujasiriamali.