Orkonerei FM

Millya amemteua Ole Njidai kuwa katibu wa ofisi ya mbunge ukanda wa Terrat

12 December 2025, 9:24 am

Picha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mbunge wa Simanjiro, James Ole Milya

Na mwandishi wetu Evanda Barnaba

Naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki na mbunge wa jimbo la simanjiro James Ole Milya amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa uteuzi wake wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka jamii ya kifugaji, Uteuzi huu umeonekana kama hatua muhimu katika kuonyesha ushirikiano wa serikali kwa makundi ya kijamii pia na kumtambulisha katibu wake kwa upande wa simanjiro ndugu Papaye Ole Njidai.

Sauti ya Mbunge wa Simanjiro, James Ole Milya

Picha katibu wa Mbunge Simanjiro proper Papaye Ole Njidai.

Katibu wa Ubunge wa Wilaya ya Simanjiro, Ndg. Ole Njidai, amemhakikishia Mbunge wa Simanjiro,kuwa atapokea na kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na mbunge kwa niaba ya wananchi wa jimbo la simanjiro

Sauti ya katibu wa Mbunge Simanjiro proper Papaye Ole Njidai.

Wananchi wa Wilaya ya Simanjiro wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, kwa maamuzi yake ya kuimarisha ushirikiano na ofisi ya Katibu wa Ubunge kwa Ukanda wa Simanjiro, akisema kuwa hatua hiyo itachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya wilaya hiyo. Wananchi wamesema kuwa kuwepo kwa Katibu katika ukanda wa Simanjiro kutaongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuharakisha utoaji wa huduma muhimu kwa jamii.

Sauti ya baadhi ya wananchi Kata ya Terrat Wilayani Simanjiro wakitoa maoni yao