Orkonerei FM

Osim Women Organization: Malezi ya Vitisho na Hasira Yanaharibu Mustakabali wa Watoto

19 May 2026, 1:44 pm

Na Baraka Olemaika

Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto kutoka shirika la Osim Women Organization, Bi. Christina Solomoni Lekui, ametoa wito kwa wazazi kubadili mfumo wa malezi na kuachana na matumizi ya nguvu au vitisho, akisisitiza kuwa njia hiyo inajenga hofu badala ya uaminifu kwa watoto. Bi. Christina amebainisha kuwa malezi bora yanapaswa kujikita katika upendo, maelewano, na kuweka mazingira yatakayomfanya mtoto awe huru kutoa taarifa na kusikiliza ushauri.

picha na mtandao(picha ya wanawake wa jamii ya kifugaji)

Akizungumza na Orkonerei Fm Radio mapema leo kwenye kipindi cha Watoto na jamii, Bi. Christina amebainisha kuwa malezi bora yanapaswa kujikita katika upendo, maelewano, na kuweka mazingira yatakayomfanya mtoto awe huru kutoa taarifa na kusikiliza ushauri.

Msikilize hapa Bi. Christina Solomoni Lekui akifafanua zaidi,