Orkonerei FM
Orkonerei FM
9 September 2025, 3:11 pm

Na Dorcas Charles
Simanjiro- Manyara
Afisa Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Simanjiro Bwana Faustine Mushi ametoa elimu kwa wananchi kuhusu namna vitendo vya rushwa vinavyojitokeza wakati wa uchaguzi na jinsi ya kuripoti pale vinapotokea.
Kwa mujibu wa Afisa huyo, rushwa za uchaguzi hujitokeza kwa sura mbalimbali ikiwemo wagombea au wafuasi wao kutoa pesa, zawadi, vyakula kwa lengo la kushawishi wapiga kura.
Aidha, TAKUKURU imewahimiza wananchi au wagombea kuripoti vitendo hivyo mara moja kwa msajili wa vyama vya siasa au kwa mwananchi wa kawaida unaweza kutoa taarifa kupitia namba za bure 113, au kufika katika ofisi za taasisi hiyo au kwa kuandika barua pepe, ili hatua za kisheria zichukuliwe mapema.
karibu kusikiliza mahojiano hayo yaliyofwanywa na mwandishi wetu Dorcas Charles