Orkonerei FM

Wazazi wafanye nini kipindi hiki cha likizo?

9 June 2026, 1:36 pm

Picha ikiwaonyesha baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Terrat, Picha na Joyce Elius

Wazazi na walezi wametakiwa kutenga muda wa kuwasimamia watoto wao kujisomea na kuwafundisha kazi za nyumbani katika kipindi hiki cha likizo, ili kuwajenga kuwa kizazi bora cha baadaye.

Na Dorcas Charles

Ushauri huo umetolewa leo na Mwalimu wa Shule ya Msingi Terrat Simanjiro, Elinema Kimambo, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Amsha Amsha kinachorushwa na Orkonerei FM Radio.

Mwalimu Kimambo amesisitiza kuwa wazazi wana wajibu mkubwa wa kufuatilia ripoti za maendeleo ya taaluma wanazopewa wanafunzi wanapofunga shule. Amesema ripoti hizo ndizo zitakazowaongoza wazazi kujua maeneo ambayo mtoto anahitaji msaada zaidi wa kimasomo akiwa nyumbani.

Mwandishi wetu Dorcas Charles amefanya mahojiano ya kina na Mwalimu Kimambo, na hapa anatuletea maelezo kamili ya kile alichokizungumza…

Sauti ya Mwalimu Kimambo