Orkonerei FM

AI inavyotumika na namna Tanzania inavyojipanga matumizi salama na yenye tija

19 June 2026, 8:00 am

Picha kwa msaada wa Mtandao.

Tanzania inaendelea kuchukua hatua katika matumizi ya Akili Bandia (Artificial Intelligence) kama sehemu ya juhudi za kuimarisha elimu, biashara, huduma za jamii na uchumi wa kidijitali. Makala hii ya sauti inaangazia namna Serikali inavyojenga mazingira ya matumizi ya AI kupitia mifumo ya kitaifa ikiwemo maendeleo ya Teknolojia ya Kiswahili, huku vijana, wafanyabiashara na taasisi mbalimbali wakitumia teknolojia hii kuongeza ufanisi katika shughuli zao za kila siku.

Na Isack Dickson

Makala hii inaangazia safari ya Tanzania katika mapinduzi ya Akili Bandia na namna teknolojia hii inavyoweza kusaidia maendeleo ya nchi katika sekta mbalimbali.

Kupitia sauti za vijana wa vyuo vikuu, mfanyabiashara mdogo, mhadhiri na viongozi, makala inaonyesha namna AI inavyotumika katika kusaidia elimu, kuboresha biashara ndogo ndogo, kuongeza ufanisi wa kazi na kutoa fursa mpya kwa Watanzania.

Pia inaeleza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kujiandaa na zama za AI, ikiwemo ujenzi wa Mfumo wa Kitaifa wa Modeli Kubwa ya Lugha ya Kiswahili (Kiswahili Large Language Model) unaolenga kuhakikisha teknolojia hii inaendana na lugha, utamaduni na mazingira ya Watanzania.

Makala hii inaeleza kuwa matumizi ya AI yanaweza kuwa kichocheo cha maendeleo ya kidijitali nchini Tanzania, huku ikisisitiza umuhimu wa kuongeza ujuzi wa teknolojia, matumizi salama ya taarifa na kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata fursa ya kunufaika na mapinduzi haya ya teknolojia.. 🎧

Makala kuhusu matumizi ya AI na namna Tanzania inavyojipanga kisera na kimfumo.