Orkonerei FM

Walazimika Kubebwa Mikononi Kuvushwa Korongoni

17 March 2026, 9:51 am

Mwonekano wa korongo linalohatarisha watu kupata huduma za afya. Picha na Evanda Barnaba

Walilazimika kubeba mgonjwa kwa shida ili kuvuka korongo hilo baada ya kushindwa kupata usafiri.

Na Evanda Barnaba

Wananchi wa Kijiji cha Oldonyo, Kata ya Lemooti wilayani Monduli wamelalamikia hali mbaya ya korongo linalowaunganisha na Kijiji cha Lolkisale wakisema limekuwa hatari na kusababisha kukosekana kwa huduma muhimu hasa kipindi cha mvua.

Agnes Gavana, mkazi wa Kijiji cha Oldonyo, amesema walilazimika kubeba mgonjwa kwa shida ili kuvuka korongo hilo baada ya kushindwa kupata usafiri.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Oldonyo, Saitoti Mwatumi, amesema serikali ya kijiji imejaribu kufanya marekebisho ya muda lakini ardhi ya eneo hilo ina mmomonyoko mkubwa. Amesema tayari viongozi wa eneo hilo wamewasilisha taarifa kwa mamlaka husika ili kupata suluhisho la kudumu kama ujenzi wa daraja au kalvati katika korongo hilo.