Orkonerei FM

Upatikanaji wa maji unavyobadili maisha ya wanawake Simanjiro

24 April 2026, 1:14 pm

Muonekano wa Moja ya kisima cha maji kilichojengwa katika kijiji cha Terrat-Simanjiro Manyara na Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira (RUWASA-Simanjiro) likiwa na ukubwa wa Lita 10,000 limekamilika mwaka 2022,ambapo ndani ya Kijiji Cha Terrat kuna matanki mawili, lengo ni kurahisisha upatikanaji wa maji (Picha na Evander Barnaba).

Na Isack Dickson

Katika Wilaya ya Simanjiro, Mkoa wa Manyara, upatikanaji wa maji safi na salama unaendelea kufungua fursa mpya za maendeleo kwa wanawake.

Kupitia kilimo cha umwagiliaji, wanawake wengi sasa wanalima mbogamboga, kuongeza kipato cha familia, kuboresha lishe za kaya na kujenga ustahimilivu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

Makala hii ya sauti inachunguza jinsi uwekezaji katika sekta ya maji unavyochangia maendeleo ya kiuchumi kwa wanawake wa Simanjiro. Utasikia simulizi za wanawake walionufaika, maoni ya wataalamu wa kilimo, viongozi wa jamii pamoja na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

Sikiliza makala hii ujifunze namna upatikanaji wa maji unavyoweza kuwa zaidi ya huduma ya msingi, bali nyenzo ya kuongeza kipato, usalama wa chakula na maendeleo ya jamii.