Orkonerei FM

Wazazi Jamii za Kifugaji Watakiwa Kuwapa Watoto Kipaumbele cha Elimu Badala ya Uchungaji

21 May 2026, 1:31 pm

Picha kwa msaada wa mtandao

Wazazi na walezi, hasa kutoka katika jamii za kifugaji Wilayani Simanjiro, wameshauriwa kubadili fikra na kuwapa watoto wao kipaumbele cha elimu badala ya kuwatanguliza katika shughuli za uchungaji wa mifugo wakati wa masomo.

Na Baraka Olemaika

Ushauri huo umetolewa kufuatia kuwepo kwa changamoto ya baadhi ya watoto kukatisha masomo au kutoroka nyumbani kwa kile kinachotajwa kuwa ni ukosefu wa usimamizi thabiti kutoka kwa wazazi.

Akizungumzia hali hiyo, Mapema Leo na Baraka Olemaika kwenye Kipindi ch Watoto na jamii cha Orkonerei Fm Radio, Mtendaji wa Kata ya Emboreti, Bwana Steven Wanga, amebainisha kuwa jamii za kifugaji zinapaswa kuiga mifano ya vijana waliopo sasa ambao wamesoma na kufanikiwa kuwatoa wazazi wao kwenye umaskini kupitia elimu.

Karibu kusikiliza mazungumzo haya……

Mtendaji wa Kata ya Emboreti, Bwana Steven Wanga