Orkonerei FM
Orkonerei FM
28 May 2026, 2:11 pm
Na Dorcas Charles
Wadau wa kisheria wamesisitiza umuhimu wa wafanyakazi wa ndani kufahamu sheria za ajira na mahusiano kazini, pamoja na kuhakikisha wanakuwa na mikataba halali inayofafanua majukumu na maslahi yao kabla ya kuanza kazi.

Picha kwa msaada wa Mtandao
Sheria hizo pia zimeainisha viwango vya mishahara kulingana na mazingira ya kazi, ambapo mfanyakazi anayeishi kwa mwajiri wake anapaswa kulipwa kima cha chini cha shilingi elfu themanini, wakati yule anayetoka nje akitakiwa kulipwa shilingi laki moja na sitini.
Msaidizi wa Kisheria, Hassan Fussa, amefafanua kwa kina kuhusu utaratibu huo wa kisheria na hatua za kuchukua pale migogoro inapojitokeza, wakati alipokuwa akizungumza na Dorcas Charles kwenye kipindi cha Amsha Amsha cha Orkonerei FM; na hapa anaanza kwa kueleza namna sheria inavyowalinda wafanyakazi hao.