Orkonerei FM
Orkonerei FM
20 May 2026, 1:46 pm
Na Nyangusi Oleng’ida
Daktari mmoja wa kituo cha afya jijini Arusha anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kumzaa anayesoma darasa la saba, huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa mama mzazi kuwa mtuhumiwa ameachiwa kwa dhamana na upelelezi unasuaasua tangu tukio hilo lilipotokea Aprili 19 mwaka huu.

Mtoto huyo kwa sasa amehifadhiwa kwenye kituo cha kulelea watoto kwa usalama wake, huku akitoa kilio chake kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima, kuingilia kati ili kupata haki.
Naye mama wa mtoto ameeleza kuwa baada ya kuona mabadiliko kwa mtoto wake ndipo akamuuliza na kusema ni baba yake ndoamemfantia kitendo hicho ndipo alipoamua kuchukua hatua ya kwenda kuripoti kituo cha polisi
Baada ya tukio hilo mwandishi wetu Nyangusi Olesang’ida amezungumza na mzazi bwana Ramadhani ili kupata maoni yake