Orkonerei FM

Wataalamu Washauri Wanandoa Kushirikiana Kwenye Maamuzi ya Uzazi wa Mpango.

1 June 2026, 2:18 pm

Na Dorcas Charles

Mtaalamu wa afya kutoka Kituo cha Afya cha Terat, Asumwisie Mwaisemba, amefafanua kuwa uzazi wa mpango unahusisha mambo makuu matatu ambayo ni idadi ya watoto, umbali wa umri wa kupishana kati ya mtoto mmoja na mwingine, pamoja na aina ya njia ya uzazi wa mpango inayopaswa kutumika.

Akizungumza na mwandishi wetu, DORCAS CHARLES Mwaisemba amesisitiza kuwa uamuzi wa kutumia njia hizi unapaswa kuwa wa makubaliano ya pamoja kati ya wenzi wote wawili na sio maamuzi ya mtu mmoja pekee.

Amewataka wale wenye mizunguko inayobadilika-badilika kutafuta ushauri wa kitaalamu ili kubaini chanzo cha mabadiliko hayo na kupatiwa matibabu yatakayosaidia kuweka mzunguko wao sawa.