Orkonerei FM
Orkonerei FM
4 June 2026, 2:26 pm

Picha ikiwaonyesha Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Terrat, Picha na Joyce Elius
Mmomonyoko wa maadili na mabadiliko ya mifumo ya malezi katika zama hizi za utandawazi na mihangaiko ya kiuchumi, umezidi kutajwa kama chanzo kikubwa cha kuporomoka kwa maadili miongoni mwa watoto.
Na Joyce Elius
Tofauti na miaka ya nyuma ambapo malezi yalikuwa ni jukumu la jamii nzima, wazazi wengi wa sasa wanalalamikiwa kutenga muda mchache mno wa kukaa na kuzungumza na watoto wao, hali inayowacha wengi wao mikononi mwa walezi wa ndani au wakijilea wenyewe mitaani.
Mwandishi wetu Joyce Elius ametuandalia taarifa hii kutoka Kijiji cha Terrat Simanjiro