Orkonerei FM

Unashirikiana na kiongozi wako katika utunzaji wa vyanzo vya maji?

8 March 2024, 2:03 pm

Mwenyekiti wa kijiji cha Terrat Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.

Jamii kwa ujumla ina nafasi kubwa katika kuhakikisha vyanzo vya maji vinaendelea kutunzwa lakini kuna changamoto kadhaa ikiwemo wao wenyewe kutofahamu umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji.

Nchi yetu imejaliwa kuwa na vyanzo vya maji vya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na mito, maziwa, ardhi oevu na maji ya chini ya ardhi. Vyanzo vya maji ni rasilimali muhimu inayochangia maendeleo ya nchi, kwani tunapata maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya nyumbani na shughuli mbalimbali.

Llicha ya kuwepo na sheria za usimamizi wa vyanzo vya maji kumekuwepo na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji kutokana na kuwepo kwa shughuli za binadamu zinazofanyika pasipo kuzingatia sheria zinazosimamia mazingira na rasilimali maji.

Shughuli hizo ni pamoja na ukataji wa miti kwa ajili ya kujipatia kuni,kilimo na maogesho ya mifugo katika vyanzo hivyo NA shughuli hizo zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa vyanzo vya maji,ambapo upelekea kuwa na changamoto za upungufu wa maji na pia mabadiliko ya tabia nchi.

Karibu kusikiliza makala hii ya Nijuze radio show kufahamu mengi kususiana na utunzaji wa vyanzo vya maji