Orkonerei FM

Uhaba wa miundombinu, vifaa tiba kituo cha afya Mererani

7 December 2023, 5:36 pm

Kituo cha afya Mererani. Picha na Mwandishi wetu Joyce Elius

Kituo cha afya Merereni kilichopo kata ya Endiamutu mji mdogo wa Mererani wilayani Simanjiro kinakabiliwa na uhaba wa miundombinu na vifaa tiba hali inayosababisha wananchi wa eneo hilo kulazimika kupatia huduma za afya mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Na Baraka Ole Maika

Akizungumza na Orkonerei FM Radio, mwenyekiti wa kamati ya afya kituo cha afya Mererani Bw. Twaha Hassan Mpanda amesema kuwa changamoto hizo zinapelea wananchi kuingia gharama kwenda kununua dawa nje ya kituo.

Aidha bwana Twaha amesema kuwa ukosefu wa wodi katika kituo hicho cha afya Mererani inapelekea wagonjwa kulazwa pamoja bila kujali mgonjwa ana ugonjwa gani hali ambayo ni hatari na sio salama kwa wagonjwa.

Sauti ya Twaha Mpanda,mwenyekiti kamati ya afya kituo cha afya Mererani

Kituo cha afya mererani kinahudumia wananchi wa kata ya Endiamutu na kata za jirani zilizopo ndani ya mji mdogo wa Mererani pamoja na kata ya Naberera wilaya ya Simanjiro, Kia iliyopo wilaya ya Hai pamoja na Kata ya Malula iliyopo wilaya ya Arumeru.