Orkonerei FM

Ulinzi na doria ulivosaidia kupunguza uwindaji haramu ndani ya ushoroba wa kwakuchinja

11 January 2024, 1:45 pm

Hao ni Tembo wanaopatikana katika ushoroba wa kwakuchinja unaounganisha hifadhi ya Tarangire na ziwa Manyara

Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya mwaka 2009 imeweka bayana kuwa
wanyamapori ni sehemu ya nyara za Serikali, hivyo mtu anayetaka kutumia nyamapori
ni lazima afuate taratibu za kisheria kuipata ikiwemo kupata kibali maalum.

Uwindaji haramu siyo tu umepungua Kwakuchinja bali hata maeneo mengine ya hifadhi
za wanyamapori nchini Tanzania baada ya Serikali kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo
kuimarisha doria na kutoa elimu kwa wananchi.

kwenye kipindi hichi (makala) iliyoandaliwa na Dorcas Charles inaangazia namna doria zinzofanywa na askari katika ushoroba wa kwakuchinja umepunguza kwa kiasi kikubwa uwindaji haramu tofauti na hapo awali karibu kusikiliza.