Orkonerei FM

Ubunifu wa mashine ya kuchakata mazao aina 9 unavyowasaidia wakulima Arusha

15 December 2023, 5:56 am

Moja ya mashine iliyotengenezwa na vijana jijini Arusha yenye uwezo wa kuchakata mazao aina 9 ikiwa inafanyiwa kazi na vijana hao pamoja na mkulima. (PICHA NA IMARATECH)

Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo kupitia taarifa yake ya mwaka 2021 uzalishaji wa mazao ulikadiriwa kufikia tani mil.4 kwa mwaka lakini tani mil.1.5 hupotea kutokana na teknolojia duni.

Uchakataji wa mazao nchini hasa kwa wakulima wadogo bado imeendelea kuwa changamoto na husababisha kupotea kwa nafaka nyingi na pia katika utunzaji wake hupelekea kuharibika.

Lakini teknolojia inaendelea kuimarika siku adi siku vijana pia wanaendelea kufanya ubunifu fuatana na mwanahabari wetu Isack Dickson katika makala fupi hii akiwa jijini arusha alipokutana na vijana waliotengeneza mashine ya kuchakata mazao usikie jinsi ilivyo na matokeo bora.