Orkonerei FM

Unatoaje taarifa za rushwa kwenye kituo cha afya?

8 May 2024, 2:11 pm

Zahanati ya Terrat, iliyopo kata ya Terrat wilaya ya Simanjiro, (Picha na Baraka Ole Maika.)

Na Isack Dickson.

Kwa mujibu wa sera ya afya ya mwaka 2020 inakemea rushwa kwenye utoaji wa huduma za afya na inasisitiza uwazi, uwajibikaji na maadili katika sekta ya afya.

Bado changamoto kubwa jamii haina uelewa namna ya kuripoti vitendo vya rushwa hasa kwenye vituo vya afya.

Kaimu kamanda TAKUKURU Wilaya ya Simanjiro Bw.ADAM MBWANA amesema yapo mazingira tofauti tofauti ya kutoa na kupokea rushwa katika huduma za afya,na hivyo wanaendelea kutoa elimu kwa wanajamii haswa wa Vijijini ili kupunguza rushwa.