Orkonerei FM

Milioni 200 ujenzi wa jengo la OPD Maroroni Arusha

12 March 2022, 6:58 pm

HABARI.

NA NYANGUSI OLE SANG’IDA

Katika kipindi cha robo ya kwanza na ya pili Halmashauri ya Wilaya ya Meru imetoa Shilingi Milioni 200 fedha za mapato yake ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa Kituo hiki cha Afya.

Ujenzi unaoendelea ni ujenzi wa Jengo Hili la OPD na Jengo la Wodi ya Mama na Mtoto .

Mkurugenzi wa wa halmashauri ya meru mwalimu Zahinabu makwinya Alisema Meru inahakikisha asilimia 10 % ya mapato ya ndani ya Halmashauri inatolewa kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na wenye ulemavu ambapo katika robo ya kwanza na ya pili ya mwaka huu wa fedha 2021/2022 tumetoa Mkopo usio na riba kwa awamu mbili

Awamu ya kwanza tumetoa Mkopo wa Shilingi milioni 93 kwa vikundi 33 vya Wanawake , Vijana na wenye mahitaji maalum

Awamu ya pili tumetoa shilingi Milioni 204.4 kwa vikundi 55 vya Wanawake , Vijana na wenye ulemavu