Orkonerei FM

Terrat, Lobosireti zazindua tamasha la michezo kwa watumishi

24 May 2024, 12:43 pm

Baadhi ya watumishi wa kata ya Terrat na Kata ya Lobosireti

Na Dorcas Charles

Wafanyakazi wa Tarafa ya Terrat na Tarafa ya Lobosiret Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara wamezindua tamasha la michezo na mazoezi ya viungo kwa watumishi yaliyofanyika shule ya sekondari Lobosireti kauli mbiu ikiwa ni “michezo ni afya!afya yako mtaji wako”.

Uzinduzi huo umeudhuriwa na watumishi wa serikali na binafsi wa sekta mbalimbali na mgeni rasmi alikua ni afisa maendeleo michezo Wilaya ya Simanjiro na baadaye kushiriki michezo mbalimbali kama vile kuvuta kamba, kukimbia ndani ya magunia, kukimbiza kuku, mbio za mita 100 na mita 300 pamoja na mpira wa miguu.

Kabla yakushiriki michezo hiyo watumishi hao walitembelea kiwanda kidogo cha asali cha mama asali ambacho kinaendeshwa na kinamama na kupokelewa na mtendaji wa kata ya lobosiret pamoja na katibu wa kikundi cha mama asali.

Sauti ya mtendaji wa Kata ya Lobosireti pamoja na Katibu wa kiwanda cha Mama Asali.

Baadhi ya wafanyakazi wakiwa wametembelea kiwanda cha Mama Asali.

Baada ya kutembelea kiwanda hicho watumishi walielekea moja kwa moja shule ya Sekondari Lobosireti kwaajili yakushiriki michezo mbalimbali iliyoandaliwa kwenye tamasha hilo.

Mgeni rasmi wa uzinduzi wa tamasha hilo alitumia wasaa huo kueleza faida chache za kufanya mazoezi na kuwashauri watumishi hao kuendelea kufanya mazoezi kila wakati kwani mazoezi ni muhimu kwa afya lakini pia amewataka watendaji wa vijiji na walimu wa shule zote za msingi kuhakikisha michezo inafanyika mashuleni.

Sauti ya afisa maendeleo michezo Wilaya ya Simanjiro

Baadhi ya watumishi walioshiriki uzinduzi huu wameeleza kufurahishwa na mazoezi na michezo iliyofanyika na kuomba kuwe na muendelezo wa matukio haya ili kuendelea kufahamiana na kubadilishana mawazo.

Sauti ya baadhi ya watumishi.

Michezo ilichezeshwa kwa pande mbili upande wa tarafa ya terrati na upande wa tarafa ya lobosiret ambapo mbio za mita 100 na mita 300 tarafa ya terrat waliibuka kidedea, upande wa kukimbiza kuku lobosiret waliondoka na kuku, kuvuta kamba lobosiret waliondoka na ushindi na mpira wa miguu lobosiret walipata ushindi wa bao 3 kwa 2, na kukimbia kwenye magunia terrat waliibuka na ushindi.

Sauti ya baadhi ya watumishi

Wachezaji wa timu ya watumishi kutoka Tarafa ya Terrat wakijiandaa na mchezo wa mpira wa miguu.