Orkonerei FM

Wanajamii watakiwa kutunza miundombinu ya maji.

20 March 2024, 6:04 pm

Baadhii ya wananchi wa kijiji cha Terrat wakifwatilia kwa makini mkutano wa mkuu wa wilaya ya Simanjiro Dkt.Suleiman Serera kuelekea kilele cha wiki ya maji. (Picha na Joyce Elius).

Na Joyce Elius.

Wakaazi wa Kijiji cha Terrat wilayani simanjiro wametakiwa kutunza vyanzo vya maji pamoja na miundombinu ya maji ili iwe endelevu na kuendelea kutumiaka kwa vizazi vijavyo.

Wito huo umetolewa siku ya leo kijijini hapo katika mkutano wa hadhara mara baada ya upandaji miti na uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa maji kitongoji cha Lemkuta A ikiwa ni kuelekea kilele cha wiki ya maji  inayoadhimishwa kila mwaka machi 22.

Akizungumza katika mkutano huo mkuu wa wilaya ya Simanjiro Dkt.SULEIMAN SERERA amesema kuwa ulinzi wa miundombinu ya maji ni muhimu ili kuendelea kuwepo pia amesisitiza matumizi ya maji kwa faida za kiuchumi.

Kuhusu idadi ya wananchi waliounganishiwa maji mkuu wa Wilaya Dkt.SERERA amesema kuwa, idadi hiyo inahitajika kuongezeka kutoka 25 kwa sasa na ameitaka ruwasa kwa kushirikiana na jumuiya ya watumia maji kubuni njia rahisi ya wananchi kulipia gharama za kuunganishiwa maji majumbani.

Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya maji, wananchi wamepata nafasi ya kuuliza maswali na kupatiwa majibu ya hayo maswali yao majibu yaliyotolewa na Meneja wa RUWAS wilaya ya Simanjiro Injinia Joanes Martin.

Awali akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi,Kata ya Terrat Ndg.Soipei Koromo amewaalika wananchi wa kata ya terrat kuhudhuria katika mikutano ya kitongoji kwa kitongoji inayofanywa na mkuu wa wilaya ndani ya wilaya ya Simanjiro.