Orkonerei FM

Ujirani mwema baina ya TAWA na jamii ya Simanjiro.

27 February 2024, 4:07 pm

Mhifadhi kutoka TAWA kanda ya kaskazini Gabriel Charles akizungumza na washiriki wa kikao cha ujirani mwema kijiji cha Terrat,Simanjiro. Picha na Baraka Ole Maika.

Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania – TAWA Kanda ya Kaskazini kitengo cha ujirani, ofisi ya Ikolojia Simanjiro Lokisale wametoa elimu ya uhifadhi na manufaa yatokanayo na Wanyamapori.

Na Baraka David Ole Maika.

Akizungumza na Viongozi mbalimbali, wazee mashuhuri na wakaazi wa kijiji cha Terrat katika kikao cha ujirani mwema Mhifadhi Wanyamapori kutoka ofisi ya TAWA kanda ya kaskazini kitengo cha ujirani mwema Ikolojia ya Simanjiro Lokisale Bw Gabriel Charles amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kuzungumzia ujirani mwema baina ya TAWA na jamii.

Mhifadhi wanyamapori Gabriel Charles kutoka TAWA kanda ya kaskazini.

Baadhi ya wakaazi wa kijiji cha Terrat walioshiriki kikao hicho Isack Abraham na Godson Nduya wamesema kuwa kikao hicho kimewafahamisha mengi ikiwepo faida zitokanazo maeneo yaliyowekezwa katika kijiji chao.

Sauti wananchi wa kijiji cha Terrat, Isack Abraham na Godson Nduya.

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Terrat Bw Kone Peneti Medukenya amesema kuwa kikao hicho kimetoa nafasi kwa wananchi kufahamu TAWA na majukumu walionayo ndani ya jamii pamoja na kuwafamisha wawekezaji waliopo katika maeneo yao.

Sauti ya mwenyekiti wa Terrat Kone Peneti Medukenya.

Katika kikao hicho cha ujirani wema Mhifadhi Charles amebainisha na kutolea ufafanuzi mgawanyo wa mapato yatokana ya uwekezaji katika Kitalu cha Uwindaji cha Simanjiro Naberera kinachojumuisha kijiji cha Terrat, Nadonjukin, Komolo, Kilombero na Naberera kuwa ni 25% inayokwenda Halmashauri na dola za Marekani 5000 zitakazogawanywa kwa vijiji vilivyopo ndani ya Kitalu.