Orkonerei FM

Familia za jamii ya kimasai zabadilika katika maamuzi ya familia

9 February 2024, 10:39 am

Wapo wanaoamini kuwa ni muhimu wanawake kushiriki katika kutoa maamuzi kwenye ngazi ya familia na wengine wanaona si muhimu,wakiamini kuwa ni kinyume na mila na tamaduni za jamii ya kimaasai.

NA Baraka David Ole Maika

Jamii ya kimaasai ni jamii inayoendelea kushikilia mila tamaduni na desturi zake na moja ya desturi hiyo ni kuamini kuwa mwanamke hana nafasi katika kufanya maamuzi kwenye ngazi ya familia.

Iko mifano mingi ya familia ambazo haziwapi fursa wanawake kuwa sehemu ya maamuzi, lakini kwa sasa wanajamii wa jamii hii wapo wanaoamini kuwa mwanaume na mwanamke wana nafasi sawa kufanya maamuzi katika familia yao.

Mwanahabari wetu BARAKA DAVID OLE MAIKA ametembelea familia hii ya bwana Abraham ambayo ni moja ya familia iliyoamua kuweka usawa wa kijinsia katika utoajia wa maamuzi na kushirikiana katika kila eneo la maisha kama familia na kutuandalia taarifa hii.

Inawezeka kuwa na familia kama hizi katika jamii zenye tamaduni zinazompa mwanaume mamlaka zaidi?jibu letu sisi ni ndiyo kama imewezekana kwa familia ya Bw Abraham na Bi Sion kwanini isiwezekane kwa wengine? tupe na wewe maoni yako kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii Instagram na Facebook @orkonereifmradio.