Orkonerei FM

Ni muhimu kuwepo na uwiano wa kijinsia katika nafasi za uongozi?

16 February 2024, 8:12 am

Baadhi ya viongozi wa kitaifa katika picha ya pamoja.(picha kwa masaada wa mtandao)

Pamoja na jitihada na utekelezaji wa sera katika kuhakikisha kunapatikana usawa wa kjinsia katika nafasi za kiuongozi mashirika ya kijamii pia yananafasi kubwa mno haswa kuhamasisha jinsia ambazo hazishiriki kwa sehemu kubwa katika kutafuta nafasi hizo za kiuongozi.

Na Wanahabari Wetu.

Wilaya ya simanjiro inajumla ya kata 18, na zote hizi madiwani wa kuchaguliwa na wananchi wote kwa ujumla ni wanaume,kwa kujazia hapo katika kata ya Terrat wenyeviti wa vijiji vyote vitatu vinavyounda kata hii ni wanaume lakini hata kwenye kijiji cha Terrat wenyeviti wote wa vitongoji ni wanaume.

Hilo linaonesha hakuna usawa wa kijinsia katika nafasi za kiuongozi lakini maoni ya wanajamii wenyewe ni yapi? na viongozi wanasemaje? mashirika ya kutetea usawa wa kijinsia mikakati ni ipi? Kuna umuhimu wa kuwa na usawa wa kijinsia katika nafasi za kiuongozi?

Majibu ya maswali yote hayo yanapatikana katika makala hii ya #Nijuze radio show inayoruka kupitia Radio Orkonerei Fm kila Alhamis saa 12:00 jioni na karibu kuisikiliza hapa pia.