Orkonerei FM

Wataalam wa afya kutoka halmashauri ya wilaya ya Simanjiro na Kanada watoa huduma za afya Terrat.

21 February 2024, 7:28 pm

Zahanati ya Terrat, iliyopo kata ya Terrat wilaya ya Simanjiro, Picha na Baraka Ole Maika.

Wataalam wa afya kutoka halmashauri ya wilaya ya Simanjiro kwa kushirikiana na wataalam wa afya kutoka Kanada kupitia shirika la Africa Afya Initiative – AAI wanatoa huduma mbalimbali za afya katika zahanati ya Terrat, wilayani Simanjiro.

Na Baraka David Ole Maika.

Orkonerei FM Radio imefika katika zahanati ya Terrat na kushuhudia wananchi wake kwa waume, watoto na vijana kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya kijiji cha Terrat waliofika eneo hilo la zahanati kupata huduma.

Akizungumza na Orkonerei FM Radio, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Terrat Dr Tumaini Kamkama, amesema kuwa huduma hiyo ni msaada kwa wakazi wa Terrat na vijiji vya jirani kupata huduma zote za kimsingi za afya.

Mganga mfawidhi zahanati ya Terrat, Dr Tumaini Kamkama.

Baadhi ya wananchi waliofika zahanati ya Terrat kupata huduma Jackson Masawe na Hellena Joshua wamesema kuwa huduma zinazotolewa ni nzuri na utaratibu wa mapokezi hadi kuhudumiwa unafurahisha na inawapunguzia gharama ya kwenda mbali kutafuta huduma.

Wananchi waliofika kupata huduma, Jackson Massawe na Hellena Joshua.

Naye mkurugenzi wa shirika la Africa Afya Initiative – AAI, Bw Steven Martine amesema kuwa mpango huo wa huduma ya afya unawezeshwa na shirika la Canadian African Community Health Alliance – CACHA, kwa lengo la kupunguza mzigo wa gharama za matibabu kwa wanajamii na katika maeneo ya kutolea huduma za afya ndani ya jamii.

Sauti ya mkurugenzi wa AAI Bw Steven Martine.
Wananchi wakiendelea kupatiwa huduma na wataalam wa afya katika zahanati ya Terrat. Picha na Baraka Ole Maika.