Orkonerei FM

Makala: Bei ya mahindi katika soko la Terrat

8 December 2023, 11:09 am

Wachuuzi wa mahindi katika soko la Terrat

Wakaazi wa kijiji cha Terrat wilaya ya Simanjiro wamelalamikia hali ya mfumuko wa bei ya mahindi ulivyongezeka kwa zaidi ya asilimia 100 kutoka shilingi elfu 7,000 hadi shilingi elfu 15,000.

Na Isack Dickson.

Jamii ya wafugaji wa kijiji cha Terrat wilaya ya Simanjiro kwa sehemu kubwa wanategemea zao la mahindi kama chakula chao kikuu kwa matumizi ya familia, japo kwa wanategemea mifugo zaidi kama kitega uchumi kwa maisha yao ya kila siku.

Kupanda kwa bei ya mahindi imekuwa changamoto na mateso kwa jamii hii ya wafugaji ambao wanategemea mifugo kwa asilimia kubwa kuwaingizia kipato na mifugo wanakosa soko kutokana na hali ya ukame uliokumba maeneo ya wafugaji na kupelekea bei ya mifugo kuporomoka.