Orkonerei FM
Orkonerei FM
25 May 2026, 2:24 pm
Na Dorcas Charles

Picha ikiwaonyesha Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Terrat, Picha na Joyce Elius
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Terrat Wilayani Simanjiro Elinema Kimambo, amewaahauri walimu kufuata sheria na taratibu zilizowekwa wakati wa kutoa adhabu kwa wanafunzi shuleni.
Na mwandishi wetu
Amesisitiza kuwa adhabu zinatakiwa kutolewa kwa kibali cha mwalimu mkuu na zisizidi kiwango cha viboko vilivyopangwa, huku akibainisha kuwa adhabu kubwa zinapaswa kuandikwa kwenye daftari maalum la adhabu.
Akizungumzia na Dorcas Charles Kwenye kipindi cha Amsha Amsha cha Orkonerei Fm Radio Mwalimu Kimambo ameeleza kuwa ushirikiano wa karibu kati ya mzazi na mwalimu una mchango mkubwa katika maendeleo ya mwanafunzi na kuwashauri walimu kuacha muadhibu wanafunzi wakiwa na jazba au hasira ili wasisababishe madhara kwa wanafunzi.
karibu kusikiliza mahojiano hayo kwa undani zaidi.