Orkonerei FM
Orkonerei FM
29 May 2026, 1:31 pm
Na Dorcas Charles

Picha ya Afisa Muuguzi Msaidizi na Mkunga kutoka Kituo cha Afya cha Terat, Asumwisye Ndumwaisemba, akiwa studio za Orkonerei Fm Radio, Picha na Evanda Barnaba.
Jamii imetakiwa kuweka mazingira wezeshi na salama kwa wanawake na wasichana ili kuwawezesha kumudu vyema afya ya hedhi, ikiwa ni pamoja na kupata vifaa vya kujihifadhi kwa bei nafuu na maji safi ya kutosha. Rai hiyo imetolewa kuelekea maadhimisho ya siku ya afya ya hedhi duniani, ambapo imesisitizwa kuwa swala la hedhi ni mchakato wa kawaida wa kibayolojia unaoashiria afya njema ya uzazi na haupaswi kuleta unyanyapaa.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Orkonerei FM, Afisa Muuguzi Msaidizi na Mkunga kutoka Kituo cha Afya cha Terat, Asumwisye Ndumwaisemba, amebainisha mambo manne muhimu yanayofanya hedhi kuwa salama, ambayo ni upatikanaji wa pedi, maji safi, vyoo bora vya kujihifadhia shuleni au kazini, pamoja na mifumo sahihi ya utupaji wa taka hizo.
Tuungane na mwandishi wetu Dorcas Charles aliyefanya mahojiano na mtaalamu huyo kutoka Kituo cha Afya cha Terat, akieleza kwa kina namna mazingira salama yanavyoweza kumsaidia mwanamke kisaikolojia na kiafya.