Orkonerei FM
Orkonerei FM
22 May 2026, 5:11 pm
Na Isack Dickson

Picha inawaontesha watoto wakicheza mchezo wa BaskettBall
Mwamko wa mchezo wa mpira wa kikapu, au basketball, umezidi kushika kasi jijini Arusha, huku vijana wadogo wakionyesha vipaji vya hali ya juu kupitia programu za mitaani na mashuleni.
Hii inakuja kufuatia mafanikio ya programu ya Pamoja Basketball, ambayo inadumu kwa miaka 10 sasa, na wikendi hii inafikia tamati ya msimu wake wa tano wa Ligi ya Kuendeleza Vijana, yaani Youth Development League. Tumepata wasaa wa kuzungumza na Mwanzilishi na Kocha wa programu hiyo, Bw. Phabian Njarifu, ambaye anaanza kwa kueleza jinsi mchezo huu ulivyopokelewa kwa ukubwa tofauti na matarajio ya wengi.
Ni wazi kuwa ushirikiano na shule hizo umezalisha vipaji vingi sana. Na sasa, ligi hiyo inafikia kilele chake mwishoni mwa juma hili. Kocha Njarifu anatoa wito kwa wakazi wa Arusha kujitokeza kwenye hatua ya nusu fainali siku ya Jumamosi, na fainali kubwa siku ya Jumapili kwenye viwanja vya Ngarenaro Sports Complex, huku akibainisha ratiba kamili na nini mabingwa watapata.

Picha ya Kocha Phabian Njarifu
Fursa hii ya kukuza vipaji hailengi tu kwa wale ambao tayari wapo kwenye mashindano haya, bali iko wazi hata kwa watoto wengine ambao wangependa kuanza kujifunza mchezo huu wa mpira wa kikapu ili kuimarisha afya na vipaji vyao mapema.