Orkonerei FM
Orkonerei FM
14 November 2025, 3:17 pm

Kipindi hiki cha Kurunzi Maalum kinachambua jinsi ongezeko la minara ya simu nchini Tanzania linavyobadilisha upatikanaji wa mawasiliano, hasa vijijini.
Kwa mujibu wa TCRA, Tanzania imefikia zaidi ya minara 10,000 ya mawasiliano, huku UCSAF ikiendelea kupanua huduma vijijini kupitia miradi inayofikia zaidi ya wananchi milioni 8.5.
Kupitia simulizi, mahojiano na uchambuzi wa kitaalamu, kipindi kinaonyesha jinsi miundombinu hii inavyowezesha vijana na wafanyabiashara kutumia mitandao ya kijamii kama chanzo cha kipato badala ya burudani pekee.