Orkonerei FM

Wazazi na walezi Terrat-Simanjiro wahimiza ushirikiano wa baba na mama katika malezi bora

28 May 2026, 2:23 pm

Picha kwa msaada wa Mtandao

Na Joyce Elius

Baadhi ya wazazi kutoka Kijiji cha Terrat wilayani Simanjiro, wameshauri wazazi na walezi kutenga muda mwingi wa kukaa na watoto wao ili kuwajenga katika misingi bora ya kimadili, ufahamu, na upendo kuanzia hatua za awali za ukuaji wao.

Wazazi hao kutoka Kijiji cha Terrat, wakizungumza kupitia Orkonerei FM Radio, wameweka wazi umuhimu wa nafasi ya familia katika ustawi wa mtoto, Wakisisitizwa kuwa malezi yenye mafanikio yanahitaji uwepo na ushirikiano wa karibu kati ya baba na mama, hatua inayomsaidia mtoto kuwa na ujasiri wa kujieleza mbele ya wazazi wake.